92 Cranbourne Ave Benoni South Africa +27 73 137 0603
Follow us:

223 MWOKOZI WETU ANATUPA FURAHA DUNIANI (G)


Mwokozi wetu anatupa furaha duniani, atuongoza kwa neema na anatushibisha. Tazama, yupo pamoja nasi, neema haitaisha kamwe! Haleluya, haleluya, haleluya, Amina!

Ni vema kumpenda Mungu aliyetukomboa, vizuri kuwa mtu wake, sitapotea kamwe. Furaha yetu itabakia, ikiwa vyote vingetoweka. Haleuya, haleluya, haleluya, Amina!

Ikiwa giza mara nyingi, na jua likifichwa, na tukijaribiwa huku twajuwa ni kwa mda. Mbinguni hatutaona kamwe huzuni wala machozi tena. Haleluya, haleluya, haleluya, Amina!

Na tusisumbukie tena chakula wala nyumba, maana vyote twavipata kwa ne’ma yake Mungu. Njiani yote atuongoza aichukuwa mizingo yetu. Haleluya, haleluya, haleluya, Aminia!

Ikiwa vema huku chini kutegemea Yesu, furaha gani huko juu kuona uso wake. Tutaiona furaha tele, na utukufu hautaisha, Haleluya, haleluya, haleluya, Amina!